9.1 Tusome kwanza maandiko katika Mwanzo 9.1-29
Back to: KOZI 101: KITABU CHA MWANZO
MWANZO 9:1-29
- Mungu akambariki Nuhu na wanawe, akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi.
- Kila mnyama wa katika nchi atawaogopa ninyi na kuwahofu, na kila ndege wa angani: pamoja na vitu vyote vilivyojaa katika ardhi, na samaki wote wa baharini; vimetiwa mikononi mwenu.
- Kila kiendacho kilicho hai kitakuwa chakula chenu, kama nilivyowapa mboga za majani, kadhalika nawapeni hivi vyote.
- Bali nyama pamoja na uhai, yaani, damu yake, msile.
- Hakika damu yenu ya uhai wenu nitaitaka; na kwa mkono wa kila mnyama nitaitaka; na kwa mkono wa mwanadamu, kwa mkono wa ndugu ya mtu nitataka uhai wa mwanadamu.
- Atakayemwaga damu ya mwanadamu, damu yake huyo itamwagwa na mwanadamu, maana kwa mfano wake Mungu alimfanya mwanadamu.
- Nanyi zaeni, mkaongezeke; zaeni sana katika nchi, mkaongezeke ndani yake.
- Mungu akamwambia Nuhu, na wanawe pamoja naye, akisema,
- Mimi, tazama, nalithibitisha agano langu nanyi; tena na uzao wenu baada yenu;
- tena na kila kiumbe hai kilichoko pamoja nanyi, ndege, na mnyama wa kufugwa, na kila mnyama wa mwitu katika nchi pamoja nanyi; wote wanaotoka katika safina, hata kila kilicho hai katika nchi.
- Na agano langu nitalithibitisha nanyi; wala kila chenye mwili hakitafutwa tena kwa maji ya gharika; wala hakutakuwa tena gharika, baada ya hayo, kuiharibu nchi.
- Mungu akasema, Hii ndiyo ishara ya agano nifanyalo kati yangu na ninyi, na kila kiumbe hai kilichoko pamoja nanyi, kwa vizazi vyote hata milele;
- Mimi nauweka upinde wangu winguni, nao utakuwa ni ishara ya agano kati yangu na nchi.
- Hata itakuwa nikitanda mawingu juu ya nchi, upinde utaonekana winguni,
- nami nitalikumbuka agano langu, lililoko kati yangu na ninyi, na kila kiumbe hai katika wote wenye mwili, wala maji hayatakuwa gharika tena kuwaharibu wote wenye mwili.
- Basi huo upinde utakuwa winguni; nami nitauangalia nipate kulikumbuka agano la milele lililoko kati ya Mungu na kila kiumbe hai katika wote wenye mwili kilichoko katika nchi.
- Mungu akamwambia Nuhu, Hii ndiyo ishara ya agano nililoliweka kati yangu na wote wenye mwili walioko katika nchi.
- Wana wa Nuhu waliotoka katika safina, ni Shemu, na Hamu, na Yafethi; na Hamu ndiye baba wa Kanaani.
- Hawa watatu walikuwa wana wa Nuhu na kwa hao nchi yote ikaenea watu.
- Nuhu akaanza kuwa mkulima, akapanda mizabibu;
- akanywa divai, akalewa; akawa uchi katika hema yake.
- Hamu, baba wa Kanaani, akauona uchi wa baba yake, akawaeleza ndugu zake wawili waliokuwa nje.
- Shemu na Yafethi wakatwaa vazi, wakalitanda mabegani mwao wote wawili, wakaenda kinyumenyume, wakaufunika uchi wa baba yao; na nyuso zao zilielekea nyuma, wala hawakuuona uchi wa baba yao.
- Nuhu akalevuka katika ulevi wake, akajua mwana wake mdogo alivyomtendea.
- Akasema,Na alaaniwe Kaanani;Atakuwa mtumwa kabisa kwa ndugu zake.
- Akasema,Na atukuzwe Bwana,Mungu wa Shemu;Na kaanani awe mtumwa wake.
- Mungu akamnafisishe Yafethi,Na akae katika hema za Shemu; Na kaanani awe mtumwa wake.
- Na Nuhu akaishi baada ya ile gharika miaka mia tatu na hamsini.
- Siku zote za Nuhu zilikuwa miaka mia kenda na hamsini, akafa.
YESU.PROSHABO.COM
0