10.1 Tusome kwanza maandiko katika Mwanzo 10:1-32
Back to: KOZI 101: KITABU CHA MWANZO
MWANZO 10:1-32
- Hivi ndivyo vizazi vya wana wa Nuhu, Shemu, na Hamu, na Yafethi. Na kwao walizaliwa wana wa kiume baada ya gharika.
- Wana wa Yafethi ni Gomeri, na Magogu, na Madai, na Yavani, na Tubali, na Mesheki, na Tirasi.
- Na wana wa Gomeri ni Ashkenazi, na Rifathi, na Togama.
- Na wana wa Yavani ni Elisha, Tarshishi, Kitimu, na Warodani.
- Kwa hao nchi za pwani za mataifa ziligawanyikana kuwa nchi zao, kila moja kwa lugha yake, kwa jamaa zao, kufuata mataifa yao.
- Na wana wa Hamu ni Kushi, na Misri, na Putu, na Kanaani.
- Na wana wa Kushi ni Seba, na Havila, na Sabta, na Raama, na Sabteka. Na wana wa Raama ni Sheba, na Dedani.
- Kushi akamzaa Nimrodi, akaanza kuwa mtu hodari katika nchi.
- Alikuwa hodari kuwinda wanyama mbele za Bwana. Kwa hiyo watu hunena, Kama Nimrodi, hodari wa kuwinda wanyama mbele za Bwana.
- Mwanzo wa ufalme wake ulikuwa Babeli na Ereku, na Akadi, na Kalne, katika nchi ya Shinari.
- Akatoka katika nchi ile akaenda mpaka Ashuru, akajenga Ninawi, na Rehoboth-iri, na Kala;
- na Reseni, kati ya Ninawi na Kala, nao ni mji mkubwa.
- Misri akazaa Waludi, na Waanami, na Walehabi, na Wanaftuhi,
- na Wapathrusi, na Wakasluhi; huko ndiko walikotoka Wafilisti na Wakaftori.
- Kanaani akamzaa Sidoni, mwanawe wa kwanza, na Hethi,
- na Myebusi, na Mwamori, na Mgirgashi,
- na Mhivi, na Mwarki, na Msini,
- na Mwarvadi, na Msemari, na Mhamathi. Baadaye jamaa za Wakanaani walitawanyikana.
- Na mpaka wa Wakanaani ulianza kutoka Sidoni kwa njia ya Gerari hata Gaza; tena kwa njia ya Sodoma, na Gomora, na Adma, na Seboimu, hata Lasha.
- Hao ndio wana wa Hamu, kufuata jamaa zao, kwa lugha zao, katika nchi zao, kufuata mataifa yao.
- Naye Shemu ambaye ni baba wa wana wote wa Eberi, na ndugu mkubwa wa Yafethi, akazaliwa wana.
- Wana wa Shemu ni Elamu, na Ashuru, na Arfaksadi, na Ludi, na Aramu.
- Na wana wa Aramu ni Usi, na Huli, na Getheri, na Mashi.
- Arfaksadi akamzaa Sela, Sela akamzaa Eberi.
- Eberi akazaliwa wana wawili wa kiume; jina la wa kwanza ni Pelegi maana katika siku zake nchi iligawanyika; na jina la nduguye ni Yoktani.
- Yoktani akamzaa Almodadi, na Shelefu, na Hasarmawethi, na Yera,
- na Hadoramu, na Uzali, na Dikla,
- na Obali, na Abimaeli, na Seba,
- na Ofiri, na Havila, na Yobabi. Hao wote ndio wana wa Yoktani.
- Makao yao yalikuwa kutoka Mesha kwa njia ya Sefari, mlima wa mashariki.
- Hao ndio wana wa Shemu, kufuata jamaa zao, na lugha zao, katika nchi zao, kufuata mataifa yao.
- Hizo ndizo jamaa za wana wa Nuhu, kufuata vizazi vyao, katika mataifa yao; na kwa hao mataifa yaligawanyika katika nchi baada ya gharika.
YESU.PROSHABO.COM
0