5.1 Tusome kwanza maandiko katika Mwanzo 5.1-32
- You must enroll in this course to access course content.
Back to: KOZI 101: KITABU CHA MWANZO
MWANZO 5:1-32
- Hiki ndicho kitabu cha vizazi vya Adamu. Siku ile Mungu alipoumba mtu, kwa sura ya Mungu alimfanya;
- mwanamume na mwanamke aliwaumba, akawabariki akawaita jina lao Adamu, siku ile walipoumbwa.
- Adamu akaishi miaka mia na thelathini, akazaa mwana kwa sura yake, kwa mfano wake, akamwita jina lake Sethi.
- Siku za Adamu baada ya kumzaa Sethi zilikuwa miaka mia nane, akazaa wana, waume na wake.
- Siku zote za Adamu alizoishi ni miaka mia kenda na thelathini, naye akafa.
- Sethi akaishi miaka mia na mitano, akamzaa Enoshi.
- Sethi akaishi baada ya kumzaa Enoshi miaka mia nane na saba, akazaa wana, waume na wake.
- Siku zote za Sethi ni miaka mia kenda na kumi na miwili, akafa.
- Enoshi akaishi miaka tisini, akamzaa Kenani.
- Enoshi akaishi baada ya kumzaa Kenani miaka mia nane na kumi na mitano, akazaa wana, waume na wake.
- Siku zote za Enoshi ni miaka mia kenda na mitano, akafa.
- Kenani akaishi miaka sabini, akamzaa Mahalaleli.
- Kenani akaishi baada ya kumzaa Mahalaleli miaka mia nane na arobaini, akazaa wana, waume na wake.
- Siku zote za Kenani ni miaka mia kenda na kumi, akafa.
- Mahalaleli akaishi miaka sitini na mitano, akamzaa Yaredi.
- Mahalaleli akaishi baada ya kumzaa Yaredi miaka mia nane na thelathini, akazaa wana, waume na wake.
- Siku zote za Mahalaleli ni miaka mia nane na tisini na mitano, akafa.
- Yaredi akaishi miaka mia na sitini na miwili, akamzaa Henoko.
- Yaredi akaishi baada ya kumzaa Henoko miaka mia nane, akazaa wana, waume na wake.
- Siku zote za Yaredi ni miaka mia kenda na sitini na miwili, akafa.
- Henoko akaishi miaka sitini na mitano, akamzaa Methusela.
- Henoko akaenda pamoja na Mungu baada ya kumzaa Methusela miaka mia tatu, akazaa wana, waume na wake.
- Siku zote za Henoko ni miaka mia tatu na sitini na mitano.
- Henoko akaenda pamoja na Mungu, naye akatoweka, maana Mungu alimtwaa.
- Methusela akaishi miaka mia na themanini na saba, akamzaa Lameki.
- Methusela akaishi baada ya kumzaa Lameki miaka mia saba na themanini na miwili, akazaa wana, waume na wake.
- Siku zote za Methusela ni miaka mia kenda na sitini na kenda, akafa.
- Lameki akaishi miaka mia na themanini na miwili, akazaa mwana.
- Akamwita jina lake Nuhu, akinena, Huyu ndiye atakayetufariji kwa kazi yetu na kwa taabu ya mikono yetu katika nchi aliyoilaani Bwana.
- Lameki akaishi baada ya kumzaa Nuhu miaka mia na tisini na mitano, akazaa wana, waume na wake.
- Siku zote za Lameki ni miaka mia saba na sabini na saba, akafa.
- Nuhu alikuwa mwenye miaka mia tano, Nuhu akawazaa Shemu, na Hamu, na Yafethi.
YESU.PROSHABO.COM
0